Wednesday, 19 November 2008

Usingizi

Usingizi... Nautafuta Siupati... Si Usiku Si Mtana
Wanipita Wakati Na Mato Nimeyabana
Silali Siwafiti Na Gomba Sijatafuna

Leo Hii Ni Wiki Wallahi Sijaufumba
Na Wala Sishikiki Najifungia Na Chumba
Natafuna Mishakiki Pilau Na Kachumba

Wale Wano Fikiri Nisemayo Ni Porojo
Musitit Sukari Kwenye Wali Wa Pojo
Mutalewa Chakari Yawatoke Mikojo

Hapa Mangi Sikalimu Yatosha Naloyaamba
Na Kama Nimeshtumu Poleni Nawaomba
Mimi Sina Wazimu Nikinya Najitamba

Usingizi ... Nautafuta Siupati... Si Usiku Si Mtana

No comments:

Post a Comment